KUANZISHWA KWA KITUO CHA ELIMU YA MSINGI YA MT. MAKSIMILIANO DAR ES SALAAM TANZANIA
Kituo cha Mt. Maksimiliano (St Maximilian Education Centre), Dar es Salaam, kilianza shughuli zake rasmi mwezi wa kwanza mwaka 2008. Kituo hiki zimeanzishwa na familia moja kutoka Parokia ya Segerea na shirika la Ndugu Wadogo Wafransisko Wakonventuali na kinatarajia kuendesha shughuli za shule ya msingi na sekondari.
Usemi wetu au motto wa kituo hiki ni Elimu inayoongeza thamani! (Education that adds value!), na lengo hasa la kituo hiki ni kuinua hali ya maisha ya watu na vilevile ya nchi nzima kwa njia ya kupata elimu bora, hasa kwa wale watoto wenye uwezo mkubwa wa kiakili .
Hata hivyo, kwa sababu ya ukosefu wa msaada wa kimali kutoka katika familia, wazazi hawawezi kuwapeleka watoto wao kusoma katika shule ghali, ambapo wanaweza kupata elimu bora.
Jambo la kutoa kipaombele (au jambo la kwanza kabisa la kuzingatia) ni kujenga majengo ya shule na baadaye kuanda vifaa kwa ajili ya shule nzima kama vile vitabu, madarasa, meza ,viti ubao na kadhalika, maabara ya komputa, kununua basi ndogo kwa ajili ya kuwaleta wanafunzi shule na kuwapeleka nyumbani kwao.
Ufumbuzi huu wa mradi wa kujenga kituo cha elimu ya msingi ulianza mwezi Januari mwaka 2008 wakati watoto wa darasa la kwanza wakianza. Kwa sababu ya ukosefu wa madarasa, wanafunzi arobaini wanasoma katika darasa liliombwa kutoka shule ya chekechea ya parokia ya Segerea, Dar es salaam.
Wamiliki wa shule hii ni ndugu wa Shirika la Wafransisko Wakoventuali. Lakini katika kuendesha shule hiyo waliwaomba masista wa kimisionari wa shirika la Familia Takatifu. Masista ambao wameanza tayari kuwafundisha watoto watahusishwa vivile katika utawala wa shule hiyo.
Kwa sasa kuna masista watatu wanaofanya kazi shuleni , mmoja kutoka Zambia, mmoja kutoka Kenya na mwingine kutoka Poland.
Baadhi ya wanafunzi kutokana na umbali wanaletwa shuleni kila siku kwa basi lililochoka au la kizamani ambalo lililetwa ili kuwawezesha wanafunzi wawahi shuleni na kuweza kuanza masomo pamoja saa mbili asubuhi. Baada ya kumaliza vipindi saa tisa alasiri, wale watoto waliopo karibu na shule wanaenda nyumbani kwa miguu lakini wale waliopo mbali na shule wanapelekwa kwa basi. Hivyo tunahitaji basi lingine kwa ajili ya kuwapeleka watoto shuleni hasa wale wadogo.
Masomo yanafundishwa kwa lugha ya Kiingereza. Kila mwezi wanafunzi wanapewa majaribio ili kuakikisha na kuona maendeleo ya kitaluma ya kila mtoto anapojifunza.
Kila siku watoto wanapata milo miwili. Saa nne asubuhi watoto wanapata chai na kitafunio yaani maandazi au biskuti, Pili watoto wanapata chakula cha mchana saa saba mchana . Siku chache zijazo ujenzi wa darasa moja utaanza katika kiwanja kiliochotolewa ambacho kiko umbali wa karibia kilometa moja na nusu (1.5km) kutoka parokiani Segerea, Dar es Salaam . Kuna uhitaji wa haraka sana kumaliza jengo hilo kwa sababu mwaka ujao 2009 darasa lingine litahitajika. Kwa kutambua madhumuni ya kituo hicho ni pamoja na kuwasaidia kulipa malipo ya shule ya wale watoto ambao hawawezi kujilipia wenyewe.
Kwa hiyo, Ndugu Wadogo Wafransisko Wakonventuali wanawasihi na kuwaomba wale watu wote wenye mapenzi mema na marafiki wote kusaidia kimali ili waweze kujenga shule hiyo.
Gharama zote za kujenga shule ni Euro laki moja, hamsini na tatu elfu, mia moja na themanini (153 180). Lakini gharama ya kujenga darasa moja ni Euro elfu nane na sitini na mbili (8062).
Misaada yote ya pesa kwa ajili ya ujenzi inaweza kutumwa kwenye akaunti ifuatayo:
Akaunti ya TSH
| Bank name: | CRDB BANK LIMITED |
| Account name: | ST. MAXIMILIAN PRIMARY AND SECONDARY SCHOOL |
| Account number: | 01J1022571000 |
Dollar account:
| Bank name: | National Bank of Commerce Ltd. Arusha - Arusha Branch |
| Bank address: | P.O. Box 3004, Arusha, Tanzania |
| Account name: | Conventual Franciscan Friars (OFM Conv) |
| Account number: | 014105004246 |
| Swift code: | NLCBTZTX |
| With indication: | Donation for St. Maximilian Education Center |
Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya wale wote wanatusaidia na kuunganika nasi katika sala na misaada yao ya hali na mali.
Tunawakikishia maombi yetu ili Mungu mwema aweza kuwajalia na kuyabariki matendo yao mema hapa duniani kwa neema zake, furaha, amani na kuwajali ufalme wa milele katika utawala wake.
Pamoja na shukrani,
Ndugu wadogo Wafransisko - Tanzania
Machi Mwaka 2008
Contact friar:
Fr. Krzysztof Cieslikiewicz OFM Conv
Provincial Delegate for Tanzania
Email: krzcie@yahoo.com
Uangalie picha za darasa la I