Ukurasa wa mbele Kitabu cha wageni Mawasiliano Links Utusaidie! English version   Polska wersja     
Misheni kwa ujumla
Miito
Shule ya Mt. Maksimiliano
Mwanga
Arusha
Dar es Salaam
Morogoro

Kifransisko
Watakatifu wa Africa
Sala mbalimbali





Uzinduzi wa Custody (Vice-Province) ya mt. Maksimiliano Tanzania

Kwa sifa na utukufu wa Utatu Mtakatifu wa Mungu na pia kwa manufaa makubwa ya watu wa Mungu na Kanisa la Tanzania na kwa ukuaji wa Shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali, katika karne ya VIII ya mwanzo ya karama ya Wafransisko; Tarehe 14/08/2009 ‘Provincial Custody’ ya Mtakatifu Maksimilian Maria Kolbe Tanzania ilizinduliwa rasmi.
Ibada ya uzinduzi wa Custody hii ilifanyika Dar-es-salaam katika Uzinduzi mpya wa nyumba ya Kustodia siku ya sikukuu ya kifodini ya Mtakatifu Maksimiliano Maria Kolbe.
Mtakatifu Maksimiliano Maria Kolbe alichaguliwa kuwa msimamizi, kwanza wa misioni, miaka 20 iliyopita katika Mwaka wa 1988, na sasa ni msimamizi wa Custody hapa Tanzania. Misa Takatifu ya uzinduzi iliadhimishwa na Mwadhama Kardinali Policarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar-es-salaam. Aliadhmisha Ekaristi Takatifku ambayo ilikiwa ya kuzindua Custody na kubariki nyumba mpya ya Shirika.
Kulikuwa na wageni na wazuru wengi kutoka Kenya, Zambia, Poland walikuwepo Provincial ndugu Miroslaw Bartos, mwekahazina wa Provincial ndugu Marek Iwanski, wasaidizi wa Mhudumu Mkuu wa Shirika duniani kutoka Roma na wageni wengine kutoka Dar-es-salaam.
Custody itakuwa na ndugu 15, 10 kutoka Poland na 5 kutoka Tanzania. Watakuwa na mkutano wa kwanza wa Custody utakaoongozwa na mhudumu wetu mkuu wa shirika duniani kote ndugu Marco Taska na mhudumu msaidizi kwa upande wa Tanzania atachaguliwa kwa mara ya kwanza.
Tukishirikishana wote furaha hii, tunaomba sala zenu kwa ajili ya uzinduzi mpya wa Custody, ili kwa Sifa na Utukufu wa Mungu Tuweze kukua hapa Tanzania.

Picha za Sherehe hii:






Design by Wafransisko                                    The web site exists since October 2006 r.