Njia ya masalaba katika Poli Sing'isi - Arusha
20 March 2009
Tarehe 20 Mwezi wa Tatu katika parokia yetu ya Poli Sing'isi tulikuwa na ibada ya Njia ya Msalaba. Siku hii ilikuwa tofauti kidogo kwa sababu tulifanya ibada yetu nje ya kanisa si ndani kama kawaida. Tulianza darajani la Mt. Antoni lililo chini zaidi kuliko kanisa lenyewe lakini si mbali na kanisa. Kwa hiyo wakati tulipopanda juu tulifanana kidogo na Yesu alipobeba masalaba wake.
Uzione picha za ibada hii: